
Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Albert Chalamila.
maambukizi ya Virusi vya Corona.
Chalamila ametoa kauli hiyo wakati akizungumza na wamiliki wa Bar mkoani Mbeya ambapo wamiliki hao wamemuahidi kwamba watahakikisha wanachukua tahadhari ya ugonjwa huo, kwa kuwapatia wahudumu Barakoa pindi wanapohudumia wateja wao, pamoja na kufunga kumbi za starehe (Disko).
Kwa mujibu Mwandishi wa EATV Mbeya Grace Mwakalinga, amesema kufuatia mapendekezo hayo, ikapelekea Mkuu wa Mkoa kubadilisha agizo lake la kuzuia Bar kufanya kazi.
#HABARI Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Albert Chalamila, ametengua kauli yake ya kuzifunga baa zote ifikapo saa tatu usiku, badala yake ziendelee na shughuli kama kawaida huku tahadhari zaidi zikichukuliwa ili kukabiliana na maambukizi ya Virusi vya Corona. pic.twitter.com/kltMKSpQxC
— earadiofm (@earadiofm) April 18, 2020