
Aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Temeke, Abdalah Mtolea.
Kwa mujibu Mtolea, ni kweli Katani alikuwa moja ya rafiki zake wa karibu, pindi alipokuwa ndani ya chama hicho hali ambayo ilipelekea watu wengi kudhani huenda Mbunge huyo akatangaza nia ya kuhamia CCM kutokana na mara ya mwisho wabunge hao kuonekana pamoja.
“Mimi siwezi kusema nilimshawishi ila kila mtu ana maamuzi yake, suala la mimi kumshauri sio jukumu langu kabla sijajiuzulu sikuwa na yeye peke yake nilikuwa na watu wengi kwa hiyo maamuzi yangu hayana uhusiano na watu wengine,” amesema Mtolea.
“Anayesema mimi nimeyumba kimsimamo, nadhani anakosa cha kuelewa nini wanafanya, ningekuwa nayumba nisingekuwa nagombania chama kwa miaka 2, na niliona kwamba CUF imeshapotea”. ameongeza.
“Kuhusu Profesa Lipumba sidhani kama anatumika na serikali kwa ajili ya kuivuruga CUF bali anafanya jambo kwa maamuzi yake mwenyewe, kwa sasa mimi sio mwanachama wa CUF tena, kwa hiyo sidhani kama Lipumba anatumika.”
Novemba 15 katika mkutano wa 13 wa bunge Abdallah Mtolea alitangaza kujiuzulu nafasi yake ya Ubunge kupitia CUF na baadaye kutangaza kuhamia CCM na Jumamosi ya novemba 24 mwaka huu Abdallah Mtolea alipewa kadi ya Chama Cha Mapinduzi kwa mara ya kwanza tangu atangaze kujiunga na Chama hicho.