
Kikosi cha Simba
Simba imeingia nusu fainali baada ya kuichapa AFC Leopard mabao 2-1 huku Bandari ikiingia nusu fainali baada ya kuifunga Singida United bao 1-0.
Kuelekea mchezo wa Simba wa nusu fainali, wadau na mashabiki wa klabu hiyo wametoa mtazamo wao juu ya wachezaji wapya wanaofanya majaribio katika klabu ya Simba kupitia michuano hiyo.
Mchezaji wa zamani wa Simba, Boniface Pawasa amesema kuwa endapo klabu hiyo inategemea wachezaji hao kwaajili ya michuano ya kimataifa itakuwa imefanya matumizi mabaya ya pesa zake kwakuwa viwango vyao vinalingana na wachezaji waliopo.
Kauli ya Pawasa inaungwa mkono na baadhi ya mashabiki lakini wengi wao wakitaka wachezaji hao kupewa muda zaidi ili kuweza kupima viwango vyao.
Simba ilithibitisha kupokea wachezaji wawili, mshambuliaji Hunlede Kissimbo wa Togo na beki Mghana, Lamine Moro na kubainisha kuwa endapo watafuzu majaribio na kucheza vizuri katika mashindano ya Sportpesa, watasajiliwa kwaajili ya michuano ya kimataifa.