Jumatano , 15th Feb , 2023

Mbunge wa jimbo la Lupembe Edwin Swale amewatembelea wahanga wa mvua iliyo nyesha Febuari 6 Mwaka huu na kupokea taarifa ya Kuharibiwa zaidi ya Ekari 450 za mahindi, 25 za parachi ,mbili za maharage huku nyumba 14 zikibolewa vibaya

Kutokana na hali hiyo Mbunge swale amesema kwa kushirikiana na serikali atahakikisha wananchi hao wa kijiji cha image kata ya kidembye Wilayani njombe wanasaidiwa mbegu ya Mahindi ya muda mfupi na ngano ili wananchi wakazalishe

Tathimini ya awali ya uharibifu ulio tolewa ulibaini ekari 72 za mahindi ziliharibiwa vibaya lakini baada ya kamati ya ulinzk na usalama kutembelea mashamba yote ya wakulima ilibaini zaidi ya ekari 250/za mahindi 25 za parachichi ,mbili za maharage ziliharibiwa vibaya na mvua kubwa iliyoambatana na upepo mkali na mawe.