'Mheshimiwa Spika nataka kujua ni nani anayepanga viwango vya nauli za ndege kwa kampuni mbili zinazosafirisha watu hapa nchini kwa sababu nauli wanazotoza kwenda mwanza toka Dar es salaam na kurudi ni laki nane ambayo ni sawa na kwenda Dubai kwa ndege za mashirika mengine'. Ameuliza Ndassa.
Akijibu swali hilo Waziri wa Uchukuzi Prof. Makame Mbarawa amesema kwamba bei ya nauli za ndege hupangwa na soko ambapo husimamiwa na SUMATRA.
Aidha Waziri amesisitiza kwamba tatizo hilo serikali inalifahamu na ndiyo maana juhudi kubwa zinafanyika ili kuweza kulifufua shirika la ndege Tanzania kwa kununua ndege ambazo zitafanya bei ishuke kwa kuwa na ushindani wa biashara.