Mbunge Sugu pamoja na Katibu wa CHADEMA kanda ya Nyanda za Juu Kusini Emmanuel Masonga.
Mahakama Kuu kanda ya Mbeya, imemfutia hukumu hiyo leo Oktoba 11, 2019, kwa madai ya kwamba hukumu hiyo ilikuwa ni batili.
Sugu alifungwa katika gereza la Ruanda, Mbeya Februari 26,2018, baada ya kuhukumiwa kifungo cha miezi mitano na Mahakama ya Hakimu Mkazi Mbeya.
Baada ya kukitumikia kifungo hicho Gerezani, Sugu aliachiwa huru, baada ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli, siku ya Aprili 26, 2018, wakati wa maadhimisho ya Sikukuu ya Muungano, kutoa msamaha wa robo moja kwa adhabu ya wafungwa waliokuwa na sifa za kunufaika na msamaha huo kwa mujibu wa Katiba ya nchi.
Mbunge Sugu pamoja na Masonga, walishikiliwa na Jeshi la Polisi wakituhumiwa kutenda kosa la uchochezi, katika mkutano wao wa hadhara ambao ulifanyika Disemba 31, 2017, jijini Mbeya, ambapo jeshi hilo lilidai kuwa viongozi hao walizungumza maneno yenye kuleta chuki kati ya Serikali na wananchi.
