Mbunge wa CHADEMA, ajiuzulu na kujiunga CCM

Alhamisi , 14th Dec , 2017
Mbunge wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Dk. Godwin Oloyce Mollel ametangaza kujivua rasmi uanachama wa chama hicho na kujiuzulu nafasi yake ya ubunge.
Mollel ametangaza kujiuzulu ubunge wake kwa madai ya kwamba sasa anafurahishwa na uongozi wa Rais Magufuli katika kupigania rasilimali za nchi ya Tanzania, hivyo yeye hana sababu ya kuendelea kupingana tena na chama cha CCM. Pia ameongeza kuwa anaungana na CCM katika kuleta maendeleo maana ameona dhamira ya kweli ya Rais Magufuli katika kuleta maendeleo. Soma zaidi barua yake