
Mchezo wa mapema utapigwa kati ya Madagascar dhidi ya Sudan majira ya Saa 11:30 kamili jioni Uwanja wa Benjamin Mkapa Stadium huku mchezo wa pili utawakutanisha mabingwa mara mbili wa michuano hii, Morocco dhidi ya bingwa mtetezi Senegal katika Uwanja wa Mandela huko Uganda majira ya Saa 2:30 kamili usiku.
Mchezo wa kumtafuta mshindi wa tatu utacheza Agosti 29 Mandela National Stadium huku mchezo wa fainali utafanyika nchini Kenya Agosti 30 katika Uwanja wa Moi huko Kasarani, Nairobi. Aidha mataifa wenyeji Kenya, Tanzania na Uganda wote wametolewa katika hatua ya robo fainali licha ya kumaliza vinara wa makundi.