Kamanda wa Polisi Mkoa wa Katavi, Damas Nyanda.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Katavi, Damas Nyanda, amesema kuwa vipande hivyo vimekutwa ndani ya mfuko wa sandarusi na kuwekwa ndani ya kanisa hilo ambapo polisi walipata taarifa ya uwepo waa nyara hizo za serikali.
Kamanda Nyanda amesema watuhumiwa hao wote walikamatwa katika kitongoji cha Tombola, kijiji cha Usevia, tarafa ya Mpimbwe na kwamba vipande hivyo vilikuwa vimehifadhiwa kwa lengo la kusafirisha.
Katika hatua nyingine jeshi hilo linamshikilia mtu mmoja kwa kukutwa na jino la Simba huko katika kijiji cha Sitarike maeneo ya Ngoroka baada ya jeshi hilo kufanya operesheni maalum katika eneo hilo.
Aidha, katika msako mwingine Kamanda Damas Nyanda, amesema wanamshikilia mtu mmoja kwa kukutwa na risasi pamoja na bduki ya SMG, akiwa ameihifadhi ndani kwake.