Meya DSM adai viongozi wa Dini wamemuokoa

Jumatatu , 13th Jan , 2020

Meya wa jiji la Dar es salaam Isaya Mwita, amesema moja ya vitu ambavyo vimesaidia yeye kuendelea kusalia kwenye kiti chake cha Umeya ni maombi ya viongozi wa Dini, ambao walimuombea kabla ya kwenda kupigiwa kura kwenye kikao cha Baraza la Madiwani.

Meya wa jiji la Dar es salaam Isaya Mwita

Meya Mwita ametoa kauli hiyo wakati akizungumza na EATV na EA Radio Digital, ambapo ameeleza kuwa, kwa sasa amesema wakati wa kikao cha Baraza la Madiwani, kura za wajumbe hazikutosha na kumfanya yeye kuendelea kukaa ofisini.

Meya Mwita amesema kuwa "mimi silazimishi kukaa ofisini kama wanataka kunitoa mimi wafuate taratibu, haiwezekani watu wafoji kura baada ya kuwa na kura 17 wakasahau mmoja yuko nje ya nchi" amesema Meya wa DSM.

"Nilisema jana viongozi wa dini walifanya kazi waliniombea sana, tena nimeshangaa sana hawa watu wamefoji mchana kweupe, tena wala hawajakamatwa" ameongeza Mwita.

Tazama video kamili hapo chini.