Tangazo la John Tory limekuja muda mfupi baada ya gazeti la Toronto Star kuripoti kwamba alikuwa na uhusiano wa kimapenzi na mwanamke huyo mwenye umri wa miaka 31 ambaye hakumtaja jina.
Alisema jambo hilo lilianza wakati wa janga la UVIKO 19 na lilimalizika kwa makubaliano maalum mwaka huu.
Kiongozi huyo mwenye umri wa miaka 68 alitaja uhusiano huo kuwa ni kosa kubwa.
Katika taarifa yake Bw Tory alisema: "Ninasikitika sana, na ninaomba msamaha bila kustahili kwa watu wa Toronto, na kwa wote walioumizwa na vitendo vyangu.
"Zaidi ya yote, ninaomba msamaha kwa mke wangu, Barb na kwa familia yangu ambao nimewaangusha zaidi kuliko mtu mwingine yeyote," aliongeza.
Bw Tory alichaguliwa tena mwaka 2018 na kuhudumu kwa muhula wa tatu madarakani miaka minne baadaye.Uchaguzi mdogo baadaye utafanyika ili kuamua mrithi aliyechaguliwa wa Bw Tory.

