Rais Xi Jinping ameagiza kuanza mara moja kwa utafutaji na uokoaji kufuatia kuporomoka kwa mgodi huo siku ya leo.
Zaidi ya wafanyakazi 200 wa uokozi wamepelekwa katika eneo la tukio na mtu mmoja ameondolewa akiwa hai hadi sasa, kulingana na shirika la habari la serikali Xinhua. Mgodi huo unapatikana maeneo ya Alxa League, katika mkoa wa Ndani wa Mongolia nchini China
Kituo cha televisheni cha taifa CCTV kimesema kuanguka kwa mgodi huo kumetokea katika shimo linaloendeshwa na Kampuni ya Uchimbaji Makaa ya Mawe ya Xinjing.
Migodi katika Mongolia ya Ndani ni baadhi ya wazalishaji wakuu wa makaa ya mawe nchini China.
Ajali za madini sio jambo geni nchini China, mnamo Desemba 2020, wachimbaji 23 walifariki dunia baada ya kuvuja kwa hewa ya ukaa katika mgodi wa makaa ya mawe.
Na mnamo Januari 2021, wachimba madini 10 walipoteza maisha katika mlipuko kwenye mgodi wa dhahabu katika mkoa wa Shandong.



