Mgonjwa wa Corona nchini aomba msamaha

Jumatano , 18th Mar , 2020

Mtanzania wa kwanza kuthibitika kuwa na ugonjwa hatari unaosababishwa na Virusi vya Corona, anayejulikana kwa jina la Isabella Mwampamba, amezungumza leo kwa njia ya simu na kuwataka watanzania wasiwe na hofu na kikubwa wazidi kuchukua tahadhari ya ugonjwa huo

Isabella Mwampamba, muathirika wa kwanza wa Virusi vya Corona Tanzania.

Akizungumza leo Machi 18, 2020, kwa njia ya simu na Waziri wa Afya Ummy Mwalimu na kuomba msamaha kwa kuwa mtu wa kwanza aliyeleta maambukizi hayo hapa nchini.

"Ninawaomba msamaha kwa kuwa mtu wa kwanza wa Corona hapa Tanzania na kutengeneza taharuki nchi nzima, hali yangu inaendelea vizuri maana siumwi chochote, wito wangu watu waache kukuza jambo, huu ugonjwa upo duniani kote" amesema Isabella.

Machi 16, 2020, Tanzania ilithibitisha kisa cha kwanza cha mgonjwa wa Corona, aliyetokea nchini Ubelgiji na kutua katika Uwanja wa Ndege wa KIA.