
Mkazi mmoja wa kijiji Mwanundi kilichopo kata ya Seng'wa wilayani Maswa mkoani Simiyu aliyefahamika kwa jina la Luth Jacob (50) amehukumiwa kwenda jela miaka 30 kwa kosa la kubaka na kumsababishia ujauzito mtoto wa shemeji yake ambaye pia ni mwanafunzi wa darasa la tano mwenye umri wa miaka 15 ambaye jina lake limehifadhiwa.
Hukumu hiyo ya shauri la jinai Na.12270/2025 imesomwa katika mahakama ya wilaya ya Maswa mbele ya hakimu mkazi mfawidhi mwandamizi Enos Misana na mshatakiwa ameshtakiwa kwa kosa moja la kubaka kinyume na kifungu cha 130(1) ( 2) (e) na 131 (1) cha sheria ya kanuni ya adhabu sura ya 16 marejeo ya mwaka 2022.
Imedaiwa mahakamani hapo mhanga huyo licha ya kuwa mwanafunzi pia ni mtoto wa shemeji yake na mtuhumiwa yaan mtoto wa mdogo wake na mke wa mshtakiwa.
Jumla ya mashahidi sita na kielelezo kimoja kilitolewa na upande wa mashtaka ambacho ni PF3 na mara baada ya kutiwa hatiani na mshtakiwa alipewa nafasi yakujitetea na katika utetezi wake yeye alidai kuwa kesi hii ni ya mchongo na amebambikiziwa huku akiahadi kumwachia Mungu.