Alhamisi , 30th Mar , 2023

Shirika kanisa katoliki linalojihusisha na utoaji wa misaada kwa wahitaji CRS limesema litaendelea kutekeleza miradi mbali mbali ya kijamii likihimiza kuendelea kuwakwamua watu walioko kwenye mazingira duni.

Rai hiyo imetolewa na katibu wa baraza la maaskofu TEC charles kitima katika kuadhimisha miaka sitini ya uwepo wake nchini Tanzania ambapo amesisitiza kuwa kanisa kupitias shirika hilo litaendelea kuwashika mkono na kuwaunganisha wenye hali duni.

Amesema kwa sasa shirika hilo limechukua maeneo mengi yakiwemo afya na kilimo na kuwataka watanzania wengi kuwa na ushirikiano katika nyanja mbali mbali bila kuwepo kwa ubaguzi kufuatia serikali kuruhusu na kuweka mazingira mazuri.