
Fu Nannan, aliyeuawa na Zheng Lingyao
Fu Nannan, aliuawa kwa risasi wakati akiamua ugomvi kati ya mwanamke aitwaye Nie Mnqin, ambaye inadaiwa aliwahi kuwa kwenye mahusiano ya kimapenzi na mtuhumiwa, na mwili wake umezikwa leo Juni 26, 2022, Mikocheni Dar es Salaam.
Wakizungumza na EATV katika mazishi ya Fu mapema leo Mikocheni Dar es Salaam, wafanyakazi na wakazi wa Kitongoji cha Madodo, Mkuranga kilipo kiwanda cha marehemu wamesema mbali na fursa za ajira walizozipata marehemu amekuwa na mchango mkubwa katika maendeleo ya jamii hiyo.