
Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, SACP Lazaro Mambosasa
Kauli hiyo ameitoa hii leo Machi 17, 2021, jijini Dar es Salaam, mara baada ya kuulizwa swali la kwamba anauzungumziaje uzushi ambao umekuwa ukizushwa kwenye mitandao ya kijamii kuhusu Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Magufuli.
"Mimi sina cha kuzungumza kwa sababu mimi siyo Msemaji wa Ikulu, Msemaji wa Ikulu yupo, unaweza kumpelekea hilo swali atajibu, lakini ninachosema tu kwa Watanzania waache kuwa wazushi wa kupokea tarifa ambazo hawajazifuatilia na kujua ukweli wake, kuzisambaza na kuendelea kuvumisha uvumi ambao hauna maana viongozi wasemaje wapo anayetaka kulijua hilo awafuate viongozi wanaohusika," amesema Kamanda Mambosasa.