Jumatano , 22nd Sep , 2021

Kijana anayejulikana kwa jina la Kidaone ameimwagia petroli na kisha kuichoma moto nyumba ya Mama mzazi wa mpenzi wake iliyopo Mikanjuni Jijini Tanga usiku wa kuamkia Septemba 21, 2021, kwa kile kilichodaiwa kuwa ni wivu wa mapenzi.

Mjane aliyechomewa nyumba yake

Tukio hilo limetokea majira ya saa 8:00 usiku, ambapo wapangaji wameiomba serikali iwasaidie kupata haki zao za mali zao ambazo zimeteketea zote na moto lakini pia isimamie sheria ipasavyo ili kumnusuru mjane huyo.

Tazama video hapa chini