Ijumaa , 8th Jul , 2022

Mkuu wa mkoa wa Tanga, Adam Malima amesema Tembo wanaovamia makazi ya wananchi na kuua watu na kuharibu mazao wataondoshwa na kufungwa kola iyakayowezesha maafisa wanyama pori  kufahamu mahali walipo na kuwadhibiti.

Akizungumza kwenye mkutano wa hadhara  kata ya Mkumbara wilaya ya Korogwe Malima amesema viongozi wa makundi hayo ya Tembo watavishwa kola ili  wafahamike mahali walipo kama njia ya kudhibitiwa kurejea kwenywe makazi ya watu.

Wataalamu  wa wanyamapori kutoka hifadhi ya Taifa ya Saadan na Taasisi ya Utafiti wa Wanyama Pori TAWIRI, wamesema baada ya kuibuka kwa tembo hao jitihada mbalimbali zimeanza kufanyika.

Maeneo yanayovamiwa na tembo hao ni kata ya Mkumbara, kata ya Mkomazi wilayani Korogwe, kata ya Mnazi na kata ya  Lunguza wilayani Lushoto, na wanadaiwa kutokea hifadhi ya Mkomazi iliyopo mkoani kilimanjaro.