Alhamisi , 29th Dec , 2022

Wakala wa nishati vijijini (REA) kanda ya magharibi imemkabidhi mkandarasi mradi wa kusambaza umeme wenye thamani ya zaidi  ya shilingi billion 6.5 utakao yafikia maeneo 46  ya pembezoni mwa miji ya Nzega na Tabora

Makabidhiano ya mradi huo yamefanyika  katika ofisi ya TANESCO  kanda ya magharibi  Mkoani Tabora  ambapo  meneja uthibiti na ufatiliaji mhandisi  Yusufu Ismail  amesema mradi huo utatekelezwa kwa muda wa miezi 18 na utawafikia zaidi ya wananchi  2000

Awali mkandarasi wa mradi huo akitambulishwa  katika ofisi ya  mkuu wa mkoa wa Tabora, balozi  Dkt. Batilda Buriani  amemtaka kuhakikisha  anatoa kipaumbele cha nafasi za ajira kwa wakazi wa Tabora  pamoja na kuwapa malipo kwa wakati

Mradi huo wa kufikisha huduma ya umeme pembezoni mwa miji (PERI URBAN) unatekelezwa  chini ya mkandarasi wa ndani  kupitia kampuni ya OK ELETRICAL SERVICES LTD