Matope yaliyotapakaa kwenye makazi ya watu
Msemaji Mkuu wa Serikali, Mobhare Matinyi amesema kwamba sehemu iliyonya maji ilizua mgandamizo na sehemu ya mlima kushindwa kuhimili na kusababisha kumeguka kwa sehemu hiyo ambayo ilitengeneza tope lililoanza kuporomoko na kuanza kuzoa mawe na miti na kwenda kushambulia makazi ya wananchi katika maeneo hayo.
Aidha ameongeza kuwa serikali ilifuatilia taarifa za matetemeko kuanzia Septemba mwaka huu hadi siku ya tukio na kubaini kuwa hakukuwa na tetemeko lolote wala mlipuko wa volkano.