
Picha ya eneo lililoteketea kwa moto
Moto unadaiwa kutokana na mafuta ya petroli yaliyokuwa yamehifadhiwa katika nyumba kulipuka.
Kaimu mkuu wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji wilaya ya Bukoba, Abdulahiman Ngaugia amesema kuwa walipata taarifa za nyumba hizo mali ya Abduswamadu Kalokola na Frederick Mtoka kuteketea kwa moto jana saa 11:30 jioni na kuwahi eneo la tukio, na kufanikiwa kupunguza madhara kwa kuzima moto huo kabla haujaenea zaidi, katika nyumba nyingine.
Kufuatia tukio hilo ambalo mbali na kuteketeza mali halikusababisha kifo au majeruhi, jeshi la zimamoto na uokoaji baada ya kuzima moto huo, walitoa elimu kwa wakazi wa eneo hilo na kuwataka kuchukua tahadhari ili kupunguza ajali za moto.