Ijumaa , 12th Sep , 2025

Kwa mujibu wa hukumu ya Mahakama kupitia kwa Jaji Jaji Abdi Kagomba, zuio lililowekwa katika shauri Na. 21692/2025, INEC Agosti 27, 2025, kuhusu kesi ya Mpina kurejesha fomu ya urais, lilikuwa kinyume cha sheria na Katiba.

Mgombea wa kiti cha Rais kupitia Chama cha ACT Wazalendo Luhaga Mpina na Makamu wa Rais, Bi. Fatma Ferej Tume watarejesha fomu za uteuzi wa kuwania nafasi hizo kesho Jumamosi, Septemba 13, 2025, saa nne asubuhi, katika ofisi za tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC)  jijini Dar es Salaam.


Taarifa ya Kaimu Mkurugenzi wa Uchaguzi, Juma Rahisi kwenda kwa Katibu Mkuu wa ACT Wazalendo, Ado Shaibu imewataka wagombea kuzingatia masharti ya Kanuni ya 20(4) ya Kanuni za Uchaguzi wa Rais, Wabunge na Madiwani za mwaka 2025 ikiwemo kuwasilisha fomu zilizojazwa kikamilifu, picha nne za rangi zenye mandhari meupe, uthibitisho wa malipo ya dhamana ya Shilingi milioni moja, na fomu namba 10 ya tamko la kuheshimu na kutekeleza maadili ya uchaguzi.



Aidha, Tume imeelekeza mgombea kuambatana na watu wasiozidi kumi (10) pekee, bila shamrashamra au maandamano ndani au nje ya jengo la tume. Uamuzi wa INEC unafuatia  hukumu ya Mahakama Kuu, Masjala Kuu Dodoma, kuamua kuwa Mpina ana haki ya kuendelea na mchakato wa kurejesha fomu ya kugombea Urais wa Tanzania.




Kwa mujibu wa hukumu ya Mahakama kupitia kwa Jaji Jaji Abdi Kagomba, zuio lililowekwa katika shauri Na. 21692/2025, INEC Agosti 27, 2025, kuhusu kesi ya Mpina kurejesha fomu ya urais, lilikuwa kinyume cha sheria na Katiba.