
Naibu Waziri wa Kilimo Anthony Mavunde akizindua mradi huo amesema utasaidia katika kudhibiti visumbufu vigeni kwa kuhakikisha mazao yanayoingia au kutoka nchini yanakuwa na ubora unaokidhi viwango vya kimataifa
Awali Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Afya ya Mimea na Viuatilifu nchini TPHPA Dkt. Efraim Njau amesema sekta ya kilimo imeajiri zaidi ya asilimia 67 ya Watanzania na kuchangia takribani asilimia 29 ya pato la taifa huku mwakilishi mkazi wa FAO Nyebenyi Tipo amesema mradi huo unalenga kuhakikisha usalama wa chakula hasa mazao