Jumatano , 11th Dec , 2019

John Justine Pambalu amechaguliwa kuwa Mwenyekiti mpya wa Baraza la Vijana la CHADEMA, akichukua nafasi ya Patrick Ole Sosopi, ambaye uongozi wake umefikia ukomo.

John Justine Pambalu amechaguliwa kuwa Mwenyekiti mpya wa Baraza la Vijana la CHADEMA.

Uchaguzi huo wa BAVICHA umefanyika usiku wa kuamkia leo Desemba 11, 2019, katika Ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam, ambapo katika Uchaguzi huo Pambalu alipata kura 150.

Akitangaza matokeo hayo Msimamizi wa Uchaguzi huo Sylvester Masinde, amesema kuwa "cha kushukuru Mwenyekiti wenu amepata Makamu Wenyeviti kutoka jinsia zote mbili kutoka Bara na Zanzibar".

Katika nafasi ya Makamu Mwenyekiti Tanzania Bara, imechukuliwa na Moza Ally Mushi, huku kwa upande wa Zanzibar, nafasi hiyo ikichukuliwa na Omary Nassoro.