Jumanne , 4th Aug , 2020

Msajili wa Vyama vya Siasa nchini Jaji Mstaafu Francis Mutungi, amekionya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), kutokana na alichokiita ni uvunjifu wa Sheria kwa kuongeza Beti la tatu kwenye wimbo wa Taifa.

Msajili wa Vyama vya Siasa nchini, Jaji Mstaafu Francis Mutungi.

Mstaafu Jaji Mutungi ametoa onyo hilo mara baada ya jana, chama hicho wakati kikiendelea na vikao vya kupitisha jina la atakaye peperusha bendera ya chama hicho katika nafasi ya Urais kuongeza Beti hilo na kusema hakutegemea kwa chama kikongwe kufanya kitendo hicho.

Jaji Mutungi ameongeza kuwa kwa mujibu wa katiba ni kosa, huku akivikumbusha vyama vya siasa vyote vinavyoendesha michakato katika vyama vyao kukumbuka kwamba sheria hazijakwenda likizo.