
Mwanaharakati wa kihafidhina wa Marekani Charlie Kirk, mshirika mwenye ushawishi mkubwa wa Rais Donald Trump, ameuawa kwa kupigwa risasi siku ya jana Jumatano alipokuwa akizungumza katika chuo kikuu cha Utah.
Mamlaka ilisema hakuna mshukiwa yeyote aliyetiwa kizuizini baada ya shambulio hilo la adhuhuri katika chuo kikuu cha Utah Valley University huko Orem, Utah, wakati wa hafla iliyohudhuriwa na watu 3,000 kabla ya baadaye taarifa ya polisic kusema kuwa wanaume wawili walikuwa kizuizini huku mmoja akihojiwa na vyombo vya sheria, kabla ya wote wawili kuachiliwa baadaye.
Mhalifu pekee aliyeshukiwa kufyatua risasi moja iliyomuua Kirk, 31, alikuwa mbali katika paa kwenye chuo kikuu hicho kwa mujibu wa Beau Mason, kamishna wa Idara ya Usalama wa Umma ya Utah, katika mkutano wa wanahabari saa nne baadaye huku msako wa kumsaka mshambuliaji huyo ambaye gavana wa jimbo hilo amesema ametekeleza mauaji ya kisiasa ukiwa unaendelea.
Kuonekana kwa Kirk jana ilikuwa ni tukio la kwanza kati ya 15 aliyoyapanga kuyafanya maarufu kama "American Comeback Tour" katika vyuo vikuu kote nchini humo. Mara nyingi alitumia hafla kama hizo, ambazo kwa kawaida zilivuta umati mkubwa wa wanafunzi, kuwaalika waliohudhuria kufanya nao mjadala moja kwa moja.
Alikuwa sehemu ya mfumo wa ikolojia wa washawishi wa kihafidhina wanaomuunga mkono Trump - ikiwa ni pamoja na Jack Posobiec, Laura Loomer, Candace Owens na wengine - ambao walisaidia kukuza ajenda ya rais. Kirk mara kwa mara alishambulia vyombo vya habari vya kawaida na kujihusisha katika masuala ya vita vya utamaduni kuhusu rangi, jinsia na uhamiaji, mara nyingi kwa mtindo wa uchochezi.