Jumamosi , 30th Nov , 2019

Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Anthony Mtaka amesema watanzania hasa kundi la vijana hawana budi kujisahau juu ya uwepo wa Ugonja la UKIMWI badala yake wawe makini ili wasikumbane na ugonjwa huo.

Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Anthony Mtaka.

Anthony Mtaka ametoa kauli hiyo wakati akizungumza kwenye Kilele cha Siku ya Kijiji Cha Vijana iliyoandaliwa na Tume ya Kudhibiti UKIMWI TACAIDS, ambayo imefanyika mkoani Mwanza.

Mtaka amesema kuwa "Kuna ujumbe unatembea mtandaoni unasema Jinsi UKIMWI ulivyokaa kimya, unaweza kusema haupo, unatukumbusha tusijisahau sana"

Aidha Mtaka amesema kuwa "hili gonjwa la UKIMWI Rais Mstaafu Mkapa alishalitangaza kuwa gonjwa la Kitaifa ndiyo maana wanafunzi wetu kuna elimu wanapewa juu ya namna ya awali ya kujikinga na ugonjwa huu, na hata mimi mwenmyewe niliufahamu kwa mara ya kwanza nikiwa Shule ya Msingi"

Kwa upande wa Mkurugenzi wa TACAIDS Tanzania Dr Leornard Maboko amesema lengo maonesho hayo ni kuwafikia vijana na wamewafikia kwa asilimia kubwa sana.

"Walengwa wakubwa walikuwa ni vijana na vijana walifikiwa kwa ukubwa zaidi kupitia majukwaa mbalimbali ya burudani" amesema Maboko