Jumatano , 9th Mar , 2022

Kijana wa miaka 11 anaefahamika kwa jina la Hassan amesafiri km 1200 peke yake kutoka nchini Ukraine mpaka Slovakia kutafuta hifadhi akiwa na mabegi mawili, passport na namba ya simu ya ndugu zake waliokimbilia Slovakia.

Hassan baada ya kupokelewa nchini Slovakia.

Hassan alipandishwa kwenye treni na mama yake ambaye amebaki Ukraine akimuuguza bibi yake, na kusafiri umbali wa km 1200 akiwa na namba ya simu mkononi kwa ajili ya kuwasiliana na ndugu zake akifika katika mpaka wa Slovakia.

 

Hassan alifanikiwa kufika katika mpaka wa Slovakia na kupokelewa vizuri na maafisa uhamiaji na kuitwa shujaa, na kupewa chakula na vinywaji kabla ya kukutana na ndugu zake.