Jumanne , 26th Mei , 2026

Rapper Drake anaripotiwa kukataa kuingiza Album zake tatu kwenye mchakato wa kuwania tuzo za Grammy, licha ya mafanikio makubwa aliyoyapata kupitia album hizo zilizotikisa streaming platforms mbalimbali za kusikilizia muziki duniani. 

Ripoti mbalimbali zinaeleza kuwa hatua hiyo imekuja kufuatia mvutano unaodaiwa kuwepo kati ya Drake, Grammy pamoja na Universal Music Group.

 

Kwa miaka kadhaa sasa, Drake amekuwa akikosoa hadharani mfumo wa tuzo za Grammy, akidai kuwa mara nyingi hazionyeshi uhalisia wa mafanikio ya wasanii pamoja na nguvu ya muziki wao kwa mashabiki duniani.

 

Hatua yake ya kutoshiriki Grammy safari hii imezua mjadala mkubwa mtandaoni, huku mashabiki wengi wakiamini kuwa rapper huyo hana tena haja ya kuthibitishwa na tuzo hizo kutokana na mafanikio makubwa anayopata kimuziki na kibiashara.