Jumatano , 27th Apr , 2022

Mkurugenzi Mkuu wa TMDA Dkt. Adam Fimbo, amesema kwamba watumiaji wa dawa za kuongeza nguvu za kiume wapo kwenye hatari zaidi ya kupoteza maisha kwa sababu dawa hizo hupanua mishipa ya damu.

Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Dawa na Vifaa Tiba (TMDA) Dkt. Adam Fimbo

Dkt. Fimbo, amesema kwamba dawa za kuongeza nguvu za kiume zinaongoza kwa sasa kwa kununuliwa zaidi kwenye maduka makubwa ya dawa nchini.

"Watumiaji wa dawa hizi watakufa kwa sababu zinapanua mishipa ya damu, mishipa ya kichwani ikishapanuka, itapasuka na hivyo mtumiaji wa dawa hizi atakufa tu,"amesema Dkt. Fimbo.