Jumatatu , 2nd Nov , 2015

Chama cha Wananchi CUF kimesitisha ajenda yao ya kurejesha kwa wananchi mpango wa kupinga uamuzi wa Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar ZEC, kufuta matokeo ya uchaguzi baada ya juhudi za kidiplomasia kuonyesha muelekeo wa kupata ufumbuzi.

Mgombea urais wa Zanzibar kwa tiketi ya CUF, Maalim Seif Sharif Hamad.

Akiongeza na Waandishi wa Habari jana Katibu Mkuu wa Chama hicho ambaye pia ndiye Mgombea Urais wa chama hicho Visiwani Zanzibar Maalim Seif Sharrif Hamad amesema juhudi sasa zimeanza kuonekana katika kulitafutia ufumbuzi suala hilo.

Maalim Seif amesema Juhudi zinazochukuliwa na Jumuiya ya Kimataifa katika kutafuta ufumbuzi wa mgogoro huo ikiwemo umoja wa Mataifa zinaonyesha muelekeo mzuri na kuwataka wananchi kuwa watulivu wakati huu.

Hata hivyo Maalim Seif amesema kuwa kuna kikundi cha Watu wachache ambacho kimekua kikwazo kutokana na kutetea maslahi binafsi katika kutafuta muafaka wa mgogoro huo.