Jumatano , 30th Jul , 2025

Hai, Kilimanjaro – Balozi wa kampeni ya #NamthaminiNasimamaNaye, Ms. Najma Paul, ameongoza tukio maalum la kukutana na wanafunzi wa Shule ya Sekondari Mukwasa, iliyopo katika Wilaya ya Hai mkoani Kilimanjaro.

Balozi wa kampeni ya #NamthaminiNasimamaNaye, Ms. Najma Paul, amekutana na wanafunzi wa Shule ya Sekondari Mukwasa wilayani Hai, Kilimanjaro, ambapo walikabidhiwa taulo za kike 4,556 zitakazowasaidia kuhudhuria masomo bila kikwazo kwa mwaka mzima.

Kampeni hiyo, inayoendeshwa na East Africa Television na East Africa Radio, inalenga kumwezesha mtoto wa kike kupata elimu bila vizingiti vinavyotokana na hedhi. Ms. Najma alisisitiza kuwa taulo hizo ni tiketi ya matumaini na usawa kwa mtoto wa kike.

Wanafunzi na walimu walitoa shukrani kwa msaada huo, wakieleza kuwa utapunguza utoro na kuongeza ari ya masomo. Kampeni inaendelea kushirikiana na wadau mbalimbali kote nchini kuhakikisha mazingira bora ya elimu kwa mtoto wa kike.