Alhamisi , 26th Mar , 2015

Mwanamke mmoja amefariki dunia mkoani Shinyanga, aitwaye Vumilia Kulwa (21) baada ya kuuawa na mumewe akiwa nyumbani kwa wakwe zake.

Kamanda wa polisi wa mkoa wa Shinyanga, Justus Kamungisha,

Kamanda wa polisi wa mkoa wa Shinyanga, Justus Kamungisha, amesema mwanamke huyo mkazi wa kijiji cha Mwongozo kata ya Mwenge tarafa ya Nindo wilayani Shinyanga, ameuawa na mumewe, Singingi Luyengeja (30) baada ya kumkata panga kichwani na kufa papo hapo.

Kamanda amesema chanzo cha mauaji hayo ni wivu wa mapenzi baada ya Luyengeja kusadiki mkewe amekuwa na mahusiano ya kimapenzi na mwanaume mwingine ambaye hajafahamika jina lake wala makazi.

Amesema baada ya mauaji hayo yaliyofanyika nyumbani kwa wazazi wa marehemu, mtuhumiwa ametoroka kusikojulikana na polisi wanaendelea kumtafuta.

Kamugisha amesema mwanaume huyo akipatikana atafikishwa katika vyombo vya sheria ili sheria iweze kuchukua mkondo wake.