
Mkuu wa Mkoa wa Katavi, Meja Jenerali Raphael Muhuga.
Wajumbe wa kamati ya ulinzi na usalama wametembelea kaya zilizoathirika na mvua hizo ambapo wamesema jitihada za kuwasaidia wahanga zinaendelea huku wakiwataka wananchi hao kujenga nyumba bora na imara ili kuepuka madhara zaidi.
Akitoa Taarifa kwa Mkuu wa Mkoa, Mkuu wa Wilaya ya Mlele, Bi. Rechel Kasanda amesema kuwa tayari wameshaanza kuwashughulikia wahanga lakini changamoto kubwa ni ukosefu wa vifaa ikiwemo magari ya kuwafikisha majeruhi hospitali.
Aidha Bi. Kasanda ameongeza kuwa kwa sasa wanafanya tathmini ya kuweza kujua madhara halisi yaliyoweza kujitokeza katika kijiji hicho kutokana na mvua hizo.
Akizungumza na Wananchi hao Mkuu wa Mkoa wa Katavi, Meja Rafael Muhuga, amewataka wananchi hao pia kupanda miti katika eneo hilo ili kudhibiti madhara ya mvua za upepo zinazojitokeza mara kwa mara mkoani humo.