Jumapili , 16th Apr , 2023

Mamlaka ya Hali ya Hewa nchini (TMA), imewataka wananchi kuendelea kuchukua tahadhari kutokana na uwepo wa mvua kubwa inayoweza kunyesha katika mikoa ya Dar es Salaam, Pwani, Tanga pamoja na visiwa vya Unguja na Pemba.

Mvua

Taarifa hiyo imeeleza kuwa leo Aprili 18, 2023, mvua itaendelea kunyesha katika mikoa ya Ruvuma, Morogoro, Tanga, Dar es Salaam, Singida, Morogoro, Tabora, Katavi, Rukwa, Songwe, Mbeya na Iringa pamoja na visiwa vya Unguja na Pemba, 

Kufuatia hali hiyo ya mvua TMA imesema kwamba athari zinazoweza kujitokeza ni pamoja na baadhi ya makazi kujaa maji pamoja na kuathirika kwa shughuli za kiuchumi.

Aidha angalizo la mvua kubwa limetolewa katika mikoa ya Dar es Salaam, Tanga, Morogoro Pwani ikijumuisha visiwa vya Mafia pamoja na visiwa vya Unguja na Pemba.

Pia angalizo la upepo mkali vinatarajiwa kutokea katika maeneo ya mwambao wa Pwani ya Kusini ikijumuisha mikoa ya Lindi na Mtwara.

Mvua hizo zinatarajiwa kunyesha hadi Aprili 19, 2023.