Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo, Dkt Harrison Mwakyembe.
Akizungumza katika makabidhiano hayo Katibu Mkuu Wizara ya Viwanda na Biashara, Riziki Shemdoe amesema kuwa, taasisi hiyo ni muhimu katika kutunza na kulinda maslahi ya wasanii yanayotokana na kazi zao za ubunifu.
"Makabidhiano haya ni utekelezaji wa agizo la Rais Magufuli la kuitaka COSOTA kuhamia Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo kwa lengo la kuiwezesha taasisi hii kuwa karibu na wadau wenye mrengo mmoja", amesema Shemdoe.
Akizungumza mara baada ya kupokea chombo hicho Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Dkt. Hassan Abbasi, amemshukuru Rais kwa kufanya uamuzi huo mgumu na makini kwani hiki sio kilio cha wadau tu bali wasomi pia.
"Sehemu kubwa sana ya wadau wa masuala ya Haki Miliki ni Wasanii, Watunga vitabu pamoja na masuala ya vyombo vya habari hivyo COSOTA imerudi nyumbani", amesema Dkt. Abbasi.
Julai 12, Rais Magufuli akiwa Ikulu Chamwino katika hafla ya chakula cha mchana alipokula na Wajumbe wa Mkutano wa Halmashauri Kuu ya CCM, alimuagiza Waziri mwenye dhamana kabla ya kwenda kuchukua fomu ya kugombea Ubunge jimboni kwake anatakiwa awe amekwisha kamilisha suala hilo.


