Jumanne , 13th Nov , 2018

Mwanafunzi Maliki Juma (14) anayesoma Shule ya msingi Nangurukuru, wilaya ya Kilwa, Mkoani Lindi, amelazwa Hospitalini akiuguza maumivu aliyoyapata,baada ya kudondoka juu ya mti wa maembe.

Mfano wa Jengo la shule na wanafunzi.

Akizungumza na www.eatv.tv , Bibi wa mwanafunzi huyo, Mariamu Abdallah alisema Maliki alifika kwake kwa ajili ya kutaka hela ya Mtihani,lakini kwa vile hakuwa nazo, alimruhusu aangue maembe akauze na hela atakayoipata imsaidie kulipia mtihani aliouita wa kubadilisha madarasa.

"Huyu ni mjukuu wangu anaishi na kusoma Shule ya msingi iliyopo kijiji cha Nangurukuru,alikuja kwangu Somanga kuomba hela ya kwaa ajili ya mchango kutoa mchango shuleni", amesema Mariamu.

Kwa mujibu maelezo ya mwanafunzi huyo, hela hiyo ilikuwa inahitajika shuleni kwake kwaajili ya mchango wa ujenzi wa vyumba vya madarasa.

''Baada ya kukosa hela kwa bibi yangu ninaekaa nae Nangurukuru nilikwenda Somanga kwa bibi yangu huyu, lakini kwa vile hakuwa na hela aliniruhusu niangue maembe nikauze,'' amesema Maliki.

Www.eatv ilimtafuta Mkuu wa Wilaya ya Kilwa Christopher Ngumbiagai kwa ajili kuzungumzia madai hayo ambayo ni kinyume na sera ya elimu bure amesema "nalifuatalia suala hilo, na nikigundua juu ya uwepo wa suala hilo kwenye shule husika nitahakikisha wahusika wanachukuliwa hatua kali za kisheria."