
Akizungumza na EATV leo Afisa huyo wa ustawi wa jamii Jiji la Dar es salaam amesema tatizo la utekelezaji watoto kwa mkoa wa Dar es salaam ni kubwa kwani Kwa wastani kwa siku wanapokea kesi 15 za watoto kutelejezwa na baba zao
Amesema wao kama maafisa wa ustawi wa jamii wanaendelea kuelimisha jamii juu ya kuzifahamu sheria za makuzi na malezi ya mtoto Ili kulinda haki za mtoto za kupata malezi kutoka pande zote mbili za wazazi
Nao wananchi wa maeneo mbalimbali ya Jiji la Dar es salaam wakiwemo waliotelekezewa watoto na wanaume zao wameitaka serikali kusimamia sheria hiyo kwa kuwa kama utekeleza ji wake utafanyika wanaume wengi wataacha tabia hiyo