Mr Blue amefunguka hayo kupitia EATV & EA Radio Digital wakati akizungumzia masuala mbalimbali ikiwemo suala ambalo lilibuliwa hivi karibuni na Msanii Nay wa Mitego ambaye aliwadis wasanii ambao anatembea na mabaunsa wengi.
Mr Blue amesema kuwa “sihitaji baunsa kwa sababu Mitaa inanilinda na sioni sababu ya mimi kulindwa, kwanza sina chuki na mtu, washkaji wengi wananipenda ila sisemi vibaya kwa wasanii wanaolindwa ili wawe salama, labda inawapa biashara kwenye maisha yao."
"Pia kuwa au kutokuwa na ulinzi sio hoja ya msingi ila unangalia unawatumiaje hao walinzi kama kuwadhalilisha au kwa ajili ya kukulinda” amesema Mr Blue.
Amendelea kusema kama wasanii wana ulinzi ikumbukwe hata wanasiasa pia wanao na ni watu ambao wana akili timamu na wamesoma, ila anashangaa hata dada wa uchochoroni, wauza vitumbua na magazeti nao wana ulinzi.




