
Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Job Ndugai,
Spika Ndugai ametoa kauli hiyo leo Juni 10, 2021, Bungeni Dodoma, wakati akitoa pongezi kwa wanawake wote walioshiriki kufanya maandalizi ya mkutano huo, na kuwaomba wanawake wa mikoa mingine waige mfano wa wanawake wa mkoa wa Dodoma kwa jinsi walivyouandaa vizuri.
"Tunawapongeza kwa mkutano wa juzi uliohutubiwa na Mhe. Rais ulikuwa ni mkutano wa aina yake, ama kweli wanawake wa Dodoma wanaweza, tutamuomba Mhe. Rais siku nyingine aite mkutano wa wanaume tu, na sisi tu-revenge ili wanawake waone wakwetu utakavyokuwa mkubwa zaidi ya wa kwao,” amesema Spika Ndugai.