
Mkuu wa Mkoa wa Njombe Christopher Ole Sendeka
Mtumishi huyo alikuwa akifanya kazi wilayani Mafinga Mkoani Iringa, amepotea tangu tarehe 15 Januari akiwa na pikipiki yenye namba ya usajili MC 214 BZZ aina ya King Lion katika misitu ya Sao hill.
Akizungumzia kupotea kwake, Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Elisante Ole - Gabriel amesema, "ni taarifa za kusikitisha kwa kupotea kwa mtumishi mwenzetu na tunaomba familia yake iwe watulivu kwa sasa maana tumetoa taarifa kwa jeshi la polisi wanalishughulikia."
"Nashukuru msemaji wa familia ambaye ni Mkuu wa Mkoa wa Njombe Christopher Ole Sendeka kwa kutoa ushirikiano lakini pia namuomba aendelee kuituliza familia", amesema Elisante Ole-Gabriel.
Aidha Katibu Mkuu huyo amesema bado Jeshi la Polisi linaendelea kufuatilia kwa ukaribu kupotea kwa mtumshi huyo kwa kushirikiana na jeshi la polisi.