
Akizungumza ofisini kwake jijini Dar es Salaam, Makamu Mwenyekiti wa NEC, Jaji Mbarouk S. Mbarouk amesema kuwa, uteuzi huo umefanyika baada ya Tume kupokea taarifa kutoka kwa Waziri mwenye dhamana ya Serikali za Mitaa juu ya uwepo wa nafasi za Madiwani Wanawake wa Viti Maalum katika halmashauri hizo kutokana na sababu mbalimbali.
Amezitaja sababu hizo kuwa ni pamoja na waliokuwa Madiwani katika Halmashauri hizo kufariki dunia, kujiuzulu na kuvuliwa uanachama na hivyo nafasi zao kuwa wazi.
Jaji Mbarouk S. Mbarouk amewataja Madiwani walioteuliwa na vyama wanavyotoka kuwa ni Regina Willbard Lyakurwa na Beatrisi Revocatus Silayo Halmashauri ya Wilaya ya Rombo, Regina Abiudi Liffi Halmashauri ya Manispaa ya Sumbawanga na Agness Atanazi Chilulumo Halmashauri ya Manispaa ya Tunduma, wote wanatoka CHADEMA.
Wengine ni Shahara A. Alfani na Mey R. Dadi kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Tandahimba na Mwajuma Waziri Kitumpa kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Korogwe kutoka CCM.