Ijumaa , 6th Dec , 2019

Katibu Mtendaji wa Baraza la Mitihani nchini (NECTA), Dkt Charles Msonde, amesema Mtendaji yeyote wa Elimu atakayejihusisha na uvujishaji wa mitihani kwa Wanafunzi, hatobaki salama kama ambavyo fedha za Serikali zitakavyoteketea katika uandaaji wa mtihani mwingine.

Katibu Mtendaji wa NECTA Dkt Charles Msonde.

Dkt Msonde ameyabainisha hayo wakati akizungumza na watendaji mbalimbali, wakiwemo Walimu wa Shule za Msingi na Sekondari, mkoani Tabora na kutoa onyo kali kwa wale wanaojihusisha na uvujishaji wa mitihani ya Taifa.

"Mtihani ukionekana kabla ya muda wake maana yake mtihani huo unatakiwa ufutwe, Mtihani mmoja wa kidato cha 4 ukifutwa zinapotea bilioni 60, sasa ziondoke kwa mchezo mchezo, halafu wewe uliyefungua huo mtihani unafikiri utaponaje ni wajibu wetu kulitetea Taifa letu na kuhakikisha mitihani yetu inafanyika kwa uadilifu kwa kufanya hivyo elimu yetu itakuwa bora" amesema Dkt Msonde.