Ijumaa , 2nd Mei , 2014

Baraza la Mitihani Tanzania limesema kuwa upangaji wa shule katika makundi ya ubora wa ufaulu umelenga kuimarisha ubora wa elimu na kuongeza kiwango cha Elimu katika shule za msingi na sekondari.

Katibu mtendaji wa baraza la mitihani nchini Tanzania (hNECTA) Dkt Charles Msonde.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar-es-salaam Kaimu katibu metendaji wa NECTA Dkt Charles Msonde amesema kuwa utaratibu huo utaiwezesha kila shule kujitathimini yenyewe kulingana na nafasi yake kitaifa au katika kundi iliyopo.

Vilevile NECTA imeandaa vitabu vya muongozo wa upangaji wa shule katika makundi ya Ufaulu kwa madhumuni ya kuwawezesha wadau wa elimu kufahamu upangaji wa shule kwa ubora wa ufaulu unavyofanywa.