
Rais wa Awamu ya 4, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete leo Januari 18, 2020 akisajili laini yake kwa njia ya Kieletroniki
Rais Mstaafu ameshiriki zoezi hilo leo ambapo amesema hatua ya kufanya hivyo ni kufuatia kuhimizwa na mfano aliouonesha Rais Dkt. John Pombe Magufuli alipofanya mwishoni mwa mwaka 2019.
Baada ya kushiriki zoezi hilo Kikwete amesema kuwa
Nimeitikia wito wa Serikali na Mhe Rais @MagufuliJP wa kusajili laini za simu kabla ya tarehe 20 Januari, 2020. Nimekamilisha kwa kusajili laini yangu ya mwisho leo. Namshukuru Obrien kutoka @Tigo_TZ kwa kunisajili. Nawahimiza na wengine kufanya hivyo kwai siku zimebaki chache. pic.twitter.com/bZzqyn7F21
— Jakaya Kikwete (@jmkikwete) January 18, 2020
"
Mpaka sasa zimebaki siku 2.
#FAHAMU Zimebaki siku 2 kufikia mwisho wa zoezi la usajili wa laini za simu kwa njia ya Kieletroniki, ambapo mwisho ni Januari 20, 2020.@TCRA_Tz pic.twitter.com/FN6yz3yUHj
— East Africa Radio (@earadiofm) January 18, 2020