Alhamisi , 8th Oct , 2015

Wakazi wa Arusha, Kilimanjaro na Manyara jana waliendelea kupokea Wagombea Urais kupita vyama CCM,CHADEMA, na ACT-Wazalendo katika maeneo yao huku wagombea hao wakiendelea kumwaga sera zao.

Mgombea wa Urais kupitia chama cha ACT- Wazalendo Anna Mghiwira.

Mgombea wa UKAWA kupitia chama cha CHADEMA, Mh. Edward Lowassa alihutubia mikutano yake katika majimbo ya Namanga na Longido Mkoani Arusha, wakati Mgombea wa CCM, Dkt. John Magufuli aliwahutbia wakazi wa Hai na Moshi Mjini huku Mgombea wa ACT- Wazalendo Anna Mghiwira akiwa Karatu Mkoani Manyara.

Kwa nyakati tofauti wagombea hao waliweza kueleza nia walizonazo huku Mh. Lowassa akiwashutumu wale wanamtuhumu kwa matusi majukwaani huku Dkt. Magufuli akitoa maagizo kwa Halmshari ya Moshi kuhusu Wafanyabiashara na Mama Anna Mghwira akiishtumu Serikali kuzembea katika Sekta ya Utalii.

Katika hatua nyingine kwa mara ya kwanza jana mgombea urais kupita chama cha NRA Bw. Janken Malik Kasambala alizungumza na Wananchi wa Mbagala katika mkutano wake wa kwanza toka kufungulia kwa mbio za kampeni.