Jumatatu , 16th Sep , 2019

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli, ameonesha ni namna gani alishangazwa  na Mkulima aliyeishikilia Ndege ya ATCL kwa mamlaka ya Mahakama kuu ya Afrika Kusini, kwa kile alichokieleza ni wivu tu.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli

Rais Magufuli ameyabainisha hayo leo Septemba 16, 2019, wakati wa uzinduzi wa Rada ya kuongozea ndege katika anga la Tanzania, ambapo ameeleza kuwa Shirika la Ndege la Tanzania linafanya vizuri na ndio maana kuna watu wanajitokeza kuishikilia.

''Shirika letu la ndege linaendelea vizuri, ndio maana mkisikia watu wanakamata ndege zetu msishangae sana hii ni kwa sababu ndege zetu zinafanya kazi vizuri, mimi huwa naona kama kelele za chura hazimzuii Ng'ombe kunywa maji'' amesema Rais Magufuli.

Ndege ya ATCL ilikamatwa nchini Afrika Kusini mnamo Agosti 23, 2019 na iliachiwa Septemba 3 mara baada ya jopo la mawakili wa Serikali kwenda nchini humo na kushinda kesi hiyo.