Alhamisi , 23rd Jan , 2020

Waziri wa Fedha na Mipango Dkt Philip Mpango, amesema kwa Mwenyekiti wa Bodi ambaye asingeweza kuwasilisha gawio lake kwa muda uliotolewa na Rais ilikuwa afukuzwe kazi, kutokana na utovu wa nidhamu wa kudharau agizo la Mkuu wa Nchi.

Waziri wa Fedha na Mipango Dkt Philip Mpango

Waziri Mpango ameyasema hayo jijini Dodoma, mara baada ya kupokea hundi za magawio kutoka taasisi 6, ambazo zimekamilisha jumla ya shilingi bilioni 25.12, zilizotolewa kuanzia Novemba 24, 2019 mpaka leo.

Sambamba na hilo Dkt Mpango amewataka wenyeviti wa bodi, wasisubiri mpaka Mkuu wa Nchi atoe maelekezo ndipo watoe michango na gawio.

Tazama video kamili hapo chini