Jumanne , 31st Mar , 2020

Rais Mstaafu wa Serikali ya Awamu ya Nne, Dkt Jakaya Mrisho Kikwete, ameonesha kuguswa na msiba wa aliyekuwa Katibu Mkuu wa Chama cha Wananchi (CUF), Khalifa Suleiman, aliyefariki Dunia usiku wa kuamkia leo na kusema kuwa amepoteza rafiki yake wa muda mrefu.

Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne, Dkt Jakaya Mrisho Kikwete.

Dkt Kikwete ameyabainisha hayo leo Machi 31, 2020, kupitia ukurasa wake wa Twitter, na kutoa pole kwa Mwenyekiti wa chama hicho Profesa Ibrahim Lipumba pamoja na wanachama wote na kwamba wamepoteza kada wa kuaminiwa na kutumainiwa.

"Ni kweli tulikuwa pande mbili tofauti, lakini kama wanadamu tulikuwa marafiki tangu wakati tukiwa wote bungeni na hata baada ya mimi kuacha Ubunge, daima nitamkumbuka kwa moyo wake wa upendo, ukarimu, ucheshi na huruma, tuko pamoja katika majonzi na kuomboleza, tunakuombea wewe binafsi, wanachama wote wa CUF na familia ya marehemu moyo wa subira na ustahamilivu. Innalilahi Wainna Ilaihi Rajiun" ameandika Dkt Kikwete.